0

Je, unafahamu kuwa chumvi inaweza kutumika kama scrub na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia?

Matatizo ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata ngozi iliyokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kuwafanya watumie vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao.

Kwa kulitambua hilo, wataalamu wa urembo wa asili wamegundua kuwa chumvi ni scrub yenye gharama ndogo ambayo kila mtu anaweza kutumia tofauti na urembo mwingine wa ngozi.

Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanaolifahamu hili.

Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.

Mahitaji:
Chumvi ya unga kijiko kimoja kikubwa.

Jinsi ya kufanya:
Nawa uso wako kwa maji ya kawaida, chukua kitambaa laini na safi kisha chovya kwenye chumvi baada ya hapo sugua katika ngozi yako ya uso taratibu unaweza kuitumia hata mwilini.

Baada ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako kisha jisugue kwa kutumia mikono yako.

Fanya hivyo hadi utakapoona takataka za ngozi zinatoka kisha kaa kama dakika mbili.
Ukimaliza, osha kwa kutumia maji ya baridi.

Ni muhimu kufanya zoezi hili mara mbili kwa wiki kwani linasaidia kuondoa makunyanzi na kusafisha kabisa ngozi.

Post a Comment

 
Top