0


              Mchezaji wa timu ya Wood pecker akirusha mpira


Mchezaji wa timu ya Hawili fc akirusha mpira

 Moja ya changamoto ya mchezo wa leo baada ya kukosekana kibendela mahali hapa wakaamua kuweka kipande cha gazeti huki kijiti kikiungwa na mfuko.
Mchezaji wa timu ya Hawili fc akimiliki mpira 


Timu ya Hawili fc imeweza kung'ara leo agosti 22 katika hatua ya nusu fainali ligi ya Alizeti cup baada ya kuiburuza wood pecker mabao 4 kwa 1 mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi. 

Magoli ya timu ya Hawili fc yalifungwa na Faustin Ibrahim dakika ya 24,David Mahine dakika ya 34 na Lawrance Fusi aliiandikia Hawili fc goli la tatu dakika ya 43 katika kipindi cha kwanza.

Dakika ya 68 Faustin Ibrahim aliweza kuipatia Hawili fc goli la nne na dakika ya 89 Jackson Micheal aliweza kuipatia timu yake ya Wood pecker goli la kufutia machozi.

Kocha wa timu ya Wood pecker,Lukas Mandowela alisema mchezo ulikuwa mzuri na aliongeza kusema timu yake ni mara ya kwanza kushiriki kwenye ligi hivyo matokeo ameyapokea na kushiriki kwao kama ni mazoezi tosha.

Wakati kocha wa Hawili fc,Mohamedi Farijala aliimbia Liwale Blog kuwa sasa anajipanga kwa mchezo ujao kama atapangiwa na timu gani ya kucheza nayo.

Timu ya Hawili fc ni timu inayoundwa na watumishi wa Halmshauri ya wilaya ya Liwale na timu ya Wood pecker ni timu inayoundwa na maofisa wa wanyama pori katika wilaya ya Liwale.

Kesho agosti 23 kutakuwa na mchezo uingine wa nusu fainali kati ya timu ya Sido fc Vs New generation unaotarajia kuwa mkali sana kwakuwa timu zote zikiwa na upinza sana na zinatokea mtaa mmoja na ni mara ya kwanza kukutana kwenye ligi hii.

Post a Comment

 
Top