
Yale maneno hayakuwa msumali tu kwangu
na kumbe yalikuwa ya kichoma choma vibaya mno, namna nilivyokuwa nikiyaongea
nilishangaa mama machozi ya kimtoka. Nilisita kidogo kumalizia yale maneno
ambayo yalikuwa yakinitoka hata sikujua kama niliyapangilia ama la maana
niliona yanakuja kwenye kinywa changu na kuyatamka.
Nilikuwa kimya kidogo, nikiwa na
mtazama mama kwa makini, nikitaka kusema jambo tena, ila kabla sijasema. Mama
aliianza kuongea, maneno ambayo hakika sitakuja kuyasahau kabisa, najua mama
yangu alikuwa akijua nini alichukuwa anakisema.
"Criss mwanangu we ni tegemeo
langu sana kwa sasa we ndio
maisha yangu hakika mwanangu naomba uwe mbali sana na wanawake na kama utashindwa baba, kwa sababu najua sasa umekuwa mkubwa kwa sasa, basi baba yangu naomba ufanye uchaguzi sahihi. Yote kwajili ya maisha yako mwanangu nakupenda sana sipendi nikiona unapata tabu kama kaka yako Eddy.
maisha yangu hakika mwanangu naomba uwe mbali sana na wanawake na kama utashindwa baba, kwa sababu najua sasa umekuwa mkubwa kwa sasa, basi baba yangu naomba ufanye uchaguzi sahihi. Yote kwajili ya maisha yako mwanangu nakupenda sana sipendi nikiona unapata tabu kama kaka yako Eddy.
Sijui nini kilimtokea hakuwa mtu, wanawake
tulimlea vizuri sana mimi na marehemu Baba yako. katika misingi mizuri ya dini
kama tulivyokulea wewe, lakini baba kupenda hakuna mwenyewe upendo wa kimapenzi
unakujaga pasipo mwenyewe kutegemea.”, Alisita kidogo mama huku akinitazama,
nikiwa kimya tu. Macho yangu yaliweza kubainia maneno yake yalikuwa yana maana
kubwa sana katika maisha yangu.
Mama hakuishia hapo aliendelea baada
ya kunitazama kwa muda kidogo. “Siwezi kumlaumu kwa jambo hilo na jua Bibilia
inasema vyema Mungu alituleta dunia kwa jili ya mapenzi yake, nasi hatuna budi
tupendane, tuzaliane ilituijaze dunia. Ila mwanangu chunga mwanamke utayekuja
kumpenda hakikisha ni wa namna tofauti na mwenye upendo wa dhati na wewe”. Mama
akuishia hapo, mara aliniuliza swali ni nikabaki nakodoa macho huku nikiliona nilikuwa katika mtihani mzito sana katika
maisha yangu.
Sikuwa na la kujibu maana sikuwa na
jua juu ya jambo lile, halikuwa swali lingine bali lilikuwa likiwa likimuhusu
kaka Eddy. Nilitulia ndugu msikilizaji nikabaki kimya, kabisa kimya ambacho
kilifukuzwa na maneno ya mama, huku akiyatalawa mazungumzo kwa kiasi kwamba
nilibaki kuwa msikilizaji.
“Sikiliza mwanangu Criss, katika maisha ya kaka
yako Eddy yana siri nzito juu ya ndani yake, lakini kwa sasa sidhani kwa wakati
wake wa wewe kuijua siri hiyo, wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
lakini kwa sasa hivi nitakuwa na kubebesha mzigo sana na chuki zisiokuwa na sababu cha msingi mwanangu”.
lakini kwa sasa hivi nitakuwa na kubebesha mzigo sana na chuki zisiokuwa na sababu cha msingi mwanangu”.
Mama aliongea kwa hisia mno sana, maneno
yale, niliyapokea katika mtazamo ulijaaa udadisi kama kawaida yangu, sikuiacha
hiyo tabia.
Juu ya neno siri tena si siri ya kawaida ni nzito kidogo jambo hilo lilinza kuleta walakini kidogo ndani ya kichwa changu. Jambo gani lililojificha juu ya kaka Eddy?, sasa ukawa mtihani ndani ya kichwa changu huku nikihitaji majibu yenye tija juu ya jambo lile, likionenakana muhimu sana katika maisha yangu. Maana mama alishawaniambia lazima angeweza kuniambia lakini si kwa mapema kama shauku yangu ya kutaka kufahamu ilivyokuwa ikiniongoza.
____________
Jina la Irene likarudi kichwani kwangu,
ndugu msikilizaji, ni huyo Irene ambaye niliweza kufahamu kwa uchache yalikuwa
yakimuhusu japo kuwa sura yake ilishapotea siku nyingi kichwani mwangu.
Niliitaji kumfahamu zaidi Irene, nilijiapiza kufatiria mwanzo mwisho kujua kilichopo nyuma ya lile.
Niliitaji kumfahamu zaidi Irene, nilijiapiza kufatiria mwanzo mwisho kujua kilichopo nyuma ya lile.
Wakati huo nilikuwa kimya nikiendelea kumsikiliza mama alichokuwa anasema ndani ya kinywa chake, ilikuwa si kawaida kabisa kumuona mama yupo kwenye hali ile.
Kiukweli tangia kipindi chote cha likizo yangu, siku hiyo ilikuwa yupo tofauti sana hata hali ya uchangamfu ilimpotea. Jambo lile ilionekana lilimuumiza sana ndani ya moyo wake. Nilimjua mama si mtu wakupenda kuona mimi napata tabu, eti kisa kitu fulani.
Furaha yangu ndio furaha yake, huzuni
yangu ndio huzuni yake.
"Nadhani umenielewa usifikiri
chochote mwanangu Criss nipo pamoja na wewe sahau chochote kuhusu haya unajua
vyema umebakisha siku chache ufanye mtihani wako wa kumaliza elimu ya kidato
cha sita hivyo jaribu kutulia kupunguza mawazo yasio kuwa ya msingi
yatakuharibia mambo yako mwanangu umenielewa?”. Aliniuliza mama nami nikamjibua
kwa kutikisa kichwa kuonesha nimeelewa kile alichokuwa anazungumza katika yale
mazungumzo.
_____
Wakati huo muda ulishaenda sana, na
hata jua lilianza kuchoma choma na kuongeza joto mwili, kuikaribisha mchana wa
siku hiyo. Ni nyakati hizo ambazo mama
aliniaga, na kuniachia pesa kidogo ya kufanya matumizi na yeye akilielekea
kwenye mikutano yao ya kinamama.
Nirejea chumbani kwangu punde mama
aliponiacha, njaa haikuwa ikisumbua tumbo langu, ijapokuwa nilikuwa sijapata
kuingiza chochote ndani yake. Nilirudi
ndani na kujitupa kitandani kwa mara nyingine.
Nikiwa kitandani kwangu nilitulia
kimya ni kitafakari yale mama aliyoniambia muda mchache kabla ajatoweka kwenye
macho yangu. Nikiwa nayafikiria yale
mazungumzo mara nikakumbuka lile jambo la siri. Nikajiuliza mara mbili ni siri
gani hiyo?. Fikra zangu zikaonesha kunisaliti, kabla ya kuleta tumaini, tumaini
ambalo pekee fikra zangu zikinikumbusha naweza kulipata ndani ya kijitabu alichokiandika mwenyewe kaka Eddy pasipo kulewa kilikuwa na
maana gani katika maisha yangu.
Macho yangu yakaanza kukitafuta wapi nilipokuwa
nimekitupa, baada ya kumbukumbu zangu, kupotea mahala nilipokuwa nimekiweka.
Maana nilipozoea kukiweka hakikuoneka. Mwanzoni niliona haitakuwa ngumu
kukipata lakini kadri muda ulivyokuwa unaenda ndio ugumu ulizidi kuongezeka.
Nilichanganyikiwa kwa kweli ndugu msikilizaji.
Post a Comment