0




SEHEMU YA KUMI

“Vipi Eddy unamkumbuka yule mdada?”
Aliniuliza Juma, nikatafari kidogo lakini sikuwa na jibu, nikaamua kumkabili Juma.
“Hapana mimi nimeshangaa tu, akinishangaa na kunipa pole kwa yalinikuta ila nahisi ile sura si ngeni machoni mwangu” niliyatoa maneno yale huku nikimtazama kwa makini Juma. Kabla ya kuibuka na jibu lilionifanya nijione mjinga.
“Wapi wewe… yule ni Rose rafiki yake mkubwa na Irine,” alisita kidogo Juma huku akinitazama na mimi nikimtazama katika mfadhaiko.
“Pale alipokuona ameshikwa na aibu msichana mbaya sana ndugu hafai hata kidogo ndugu, na kwambia simpendi huyu msichana si mimi tu watu hawamkubali hata kidogo hapa chuo unavyoona.
Maneno yale ya Juma yaliniiingia kwenye kichwa changu akili ikaaanza kumtafuta.
“Rose… Rose!”, kama dakika kadhaa nikakumbuka yeye ndio alikuwaga msaada kwangu mpaka kujenga mazoea na Irine.  Nikaikumbuka vizuri siku ya kwanza kuonana na Irene kule cafe area yule msichana ndio alikuwepo pamoja na wenzake wakipiga domo pale karibu na meza nilipokaa mimi. 
Oooh!.. aiseeeh!... Juma nimemkumbuka huyu manzi" nilizungumza kwa hamaki.

“Basi ndugu yule msichana hafai hata kidogo….. hafai kaka hata kwa kulumagia…. acha mimi na kwambia acha babu!, mwone vile vile mnafiki tu yule asikuambie mtu ninavyokuambia unavyomuona huyo Irene wako si bure tabia zote unazozijua mbovu yule mdada ndio atakuwa anahusika. Si ndio rafiki yake mkubwa!. Siku hizi wamekuwa hawafai hata kidogo lecture gani asiyewajua hawa we kaulize?!” Juma aliongea kwa msisitizo sana yale maneno yake.
Yaliniiingia vilivyo kwenye ubongo wangu, hapo tena hata hamu ya kutaka kujua habari za Irene ziliniisha kabisa. Ingetokea wapi?, sikutaka kuutesa moyo wangu kabisa kama Mungu amenipangia kunipa basi hata nipa lakini si kwa majaribu haya alionipatia yanatosha kabisa, nilisema na moyo wangu.
Wakati huo, tulizungumza kwa kina na Juma na nilimweleza juu ya hatima yangu katika masomo. Uzuri Juma alikuwa rafiki mzuri sana kwangu hakunivunja moyo alinifaliji, nichukulie hali ile ya kawaida nisifikirie kitu kibaya umri wangu bado ulikuwa ukiruhusu kizuri sasa nipo na ninafuraha tele na mwenye afya hiko ndio kikubwa pia hakusita kunipa ushauri juu ya wanawake. Niweze kuwanao mbali kabisa na kama nitashindwa basi niangalie mwanamke wa kuanae na si wanawake wote tu. Nilimwelewa vyema na kumwahidi nitazingatia yale yote aliyoniambia.
Hakika Juma alikuwa rafiki mwema sana kwake, kuhusu yote siwezi  kumpa lawama yeye najilaumu mwenyewe na nafasi yangu.  
Muda nao haukuwa rafiki sana kwetu, baada ya zaidi ya lisaa nikiwa naendelea mazungumzo.  Mida ya kipindi kwa upande wake Juma ilikuwa ikiwadia hakuwa na jinsi ilimbidi tu aende na kutuacha mimi na Criss tukiangalia njia ya kutokea ndani ya chuo. Tulipiga hatua kwa dakika kadhaa huku nikitafakari yale niliyokutana nayo ndani ya chuo kile nikiwa nimeinamisha kichwa na kukata hatua.
Hamadi ile na nyanyuaa kichwa kwa mbali niliona kitu, kilifanya mapigo yangu ya moyo yaende mbio hata nilipojaribu kuizuia hali ile nilishangaa nikishindwa kujizuia.
Moyo nilihisi maumivu makali kweli, taswira ile niliyokuwa nikiiyona japo kwa mbali ila haikuwa ikileta hali ya kawaida ndani ya moyo wangu, ili leta mfadhahiko kwa kiasi hata ule uchangamfu niliokuwa nawo hapo awali njiani mule ulipotea.
Sura ya Irene mboni zangu ziliweza kusawili kile nilichokuwa na kiona na afadhari angekuwa yeye pekee yake, bali alikuwa na mwanaume. alivyokuwa amekamatia vizuri kuino chake. Licha ya yote ila nilishangaa tu roho inauma mbaya. Usiombe ndugu kitu ukiwa unakipenda haijalishi ikiwe kimekutenda namna gani ila bado kitabaki ndani ya moyo na kama kidonda ukikigusa basi kina shituka. Basi mimi nilishituka na ukweli niliumia sana kwa siku hiyo, na kupoteza furaha yangu kabisa.  
Hata hali ya kuendelea kupita njia ile ilinishinda kabisa miguu yangu ilijikuta inabadilisha njia huku mikono yangu ikikosa nguvu hata kuishika mikono ya mdogo wangu Criss.
__________
Nilijivuta taratibu sikutaka kuungalia hali ile niliyoina kwenye mboni ya macho yangu muda mfupi, niliendelea kufakamia ardhi taratibu huku kichwani mwangu jambo lile lilikuwa likinirudia. Hapo sasa maneno ya Juma yalianza kuingia vizuri kwa mara nyingine ndani ya kichwa changu nakuamini alikuwa sahihi asilimia zote haikuwa haja tena ya kupinga maneno yake hata kidogo unayapingaje?, kwanza alikuwa sahihi kabisa Juma kwa kile alichokuwa anakiongea. Hapo niliamini hata ule msemo wake ya kuwa kama kunavitu duniani hapa havipendeki basi ni viumbe vinaitwa wanawake.

Mawazo hayo yote yalikuwa yananigonga ni kiwa njiani kurudi
Nyumbani, hata tulivyoingia nyumbani siku jua nilishaanga tu nipo ndani nimeshika kidaftari ambacho kilikuwa kama kijitabu nilichonunua wakati tulipokuwa India na kuanza kuandika mambo yote kuanzia pale nilipoona na yule binti basi kuanzia hapo niliendelea kuandika tu hata sikujua hali ile ilikuwa ikitokea wapi?.
Naikumbuka vyema siku ile hatumkuta mama, sikujua alikuwa ameenda wapi kwa muda ule ila baadae niliweza kufahamu kumbe alikwenda sokoni. Kununua mahitaji na kwabahati nzuri mama alinunua mboga niliyokuwa naipenda. Ukweli nilifurahi sana na hata hapo mambo yakitokea chuo kwa siku ile nilianza kuyasahau kwa muda mfupi upendo wa mama nyie hakuna zaidi yake alikuwa akinifurahisha kweli. Kila siku alikuwa anapika vitu ninavyo vipenda na uzuri Criss yeye alikuwa kama mimi ninachokipenda na yeye anakipenda kasoro kwenye mboga ya maharage tu, yeye alikuwa akiyapenda sana tofauti na mimi .  
Sikuchelewa nilimueleza mama habari za chuo, alinilelewa tu vyema.
                                                     ************
Zilipita kama wiki mbili hapo, nilikuwa nahitajika kurudi tena chuoni ilikufatiria mipango yangu kama nilivyo ongea na mkuu wa shule.  Mapema tu asubuhi ya siku ile, nilianza safari ya kuelekea kule safari hii nikiwa pekee yangu tofauti na mara ya mwisho nilipoenda maeneo yale.
Baada ya muda kidogo nilifika eneo lile lakini siku ile ilikuwa tofauti kabisa walionekana watu wengi sana wakikatiza chuoni mule namna ya uvaaji wao tu ulitosha kubaini kuwa kulikuwa na bonanza siku ile ndani ya chuo. Sikutaka kufatiria habari zile sana niliendelea kukatiza mitaa kuelekea ofisini kwa mkuu wakati huo tu niliendelea kupishana na wanachuo wengine wakiwa kwenye vikundi vikundi taratibu tu nilipiga hatua zangu ila kunakitu kilinistajabisha, mpaka nikajistukia wakati na pishana na kikundi kimoja cha wadada.

Post a Comment

 
Top