0

 Mapiganao makali yameripotiwa pembezoni mwa mji mkuu wa Sudan Kusini Juba.

Makabiliano hayo ni kati ya wanajeshi wa serikali na wale wa kiongozi aliyeondolewa madarakani Riek Machar.

Mapigano hayo yamejiri wiki moja baada ya rais wa Sudan Kusini kumuapisha makamu wa kwanza mpya Taban Gai.

Wasemaji wa pande mbili wamekua wakilaumiana kwa mashambulio.

Msemaji wa SPLA Lul Ruai Koang, amesema kwamba mapigano yalishika kasi mwishoni mwa wiki, maili tisini kaskazini mashariki mwa mji mkuu Juba, baada ya mashambulizi ya makombora kutoka kwa majeshi ya upinzani kutoka maeneo matatu tofauti.

Vikosi vya upinzani kutoka SPLA vilivyojitenga na serikali vinalaumu serikali kwa kukusanya majeshi na kutuma helikopta za kivita kumsaka aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar, aliyetoroka juba vita vilipoanza.

Meja Dickson Gatluak amekiri kwamba vikosi hivyo vya upinzani vililemewa katika maeneo kadhaa ndani na viungani mwa mji mkuu Juba kwa sababu za idadi chache ukulinganisha na vikosi vya serikali

Pia ameongezea kwa kusema kwamba vikosi hivyo vya upinzani vimeelimishwa dhidi ya ukatili wa kijinsia na havihusiki katika madai yoyote ya ukatili kwa sababu vilikuwa vimeshajiondoa katika maeneo ambayo kunaripotiwa visa kama hivyo

Post a Comment

 
Top