Agosti
3, 2016 kulikuwa na taarifa za kukamatwa kwa mwanasheria ambae ni
mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akiwa kwenye mkutano wake katika
kijijini Ikungi Singida.
Sasa
basi mwanasheria huyo ameshawasili leo jioni Agosti 4, 216 Dar es
Salaam kwaajili ya mahojiano na Polisi kutokana na maneno
aliyoyazungumza Agosti 2,2016 kusadikiwa kuwa ni ya uchochezi kwa
Serikali pamoja viongozi wa nchini.
Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya kayaongea haya>>Tumeshampata
yupo na tunaendelea kumhoji kuhusiana na kauli zake alizozitoa siku ya
Agosti 2, 2016 pale Mahakamani, amefika majira ya jioni Dar es Salaam
kwahiyo tunaendelea na mahojiano kwani alitoa kashfa kwa Serikali alitoa
Kashfa kwa Kiongozi’- Polisi
‘Sasa
yeye ni Mwanasheria lakini anatoa maneno ya uchochezi kwahiyo kama
Jeshi la polisi lazima tumshurutishe ili awe makini na sheria za nchini
na mwisho wa siku baada ya mahojiano tutampeleka Mahakamani’– Polisi
Post a Comment