0


Kikosi cha Yanga kitakachoanza leo dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
1. Deogratius Munishi Dida
2. Juma Abdul Japhary
3. Haji Mwinyi Ngwali.
4. Andrew Vicent Dante
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite Junior
7. Saimon Happygod Msuva
8. Thaban Michael Kamusoko
9. Amiss Jocelyn Tambwe.
10. Obrey Cholla Chirwa
11. Deus David Kaseke


Kikosi cha akiba ni
1. Benno Kakolanya
2. Oscar Fanuel Joshua
3. Malimi Marcel Busungu
4. Haruna Niyonzima Fabregas
5. Juma Said Makapu
6. Kelvin Patrick Yondani
7. Juma Mahadhi Neymar



 Wachezaji wa timu ya Yanga wakipongezana.

HAKUNA namna, lazima ushindi upatikane leo ili kufufua matumaini ya Yanga kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Hans van Der Pluijm ameamua kuchenji gia ili kuhakikisha anapata ushindi kwa namna yoyote ile.

Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo wa tano kwao katika Kombe la Shirikisho, ikipambana na Waarabu MO Bejaia kutoka Algeria kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar lakini Pluijm ameamua kuwabadilishia kikosi na kutamba kuwa Mwarabu huyo hatoki leo Taifa.
 Waarabu MO Bejaia kutoka Algeria.

Yanga imepoteza mechi tatu na kutoka sare moja katika hatua hii. Ipo mkiani mwa Kundi A lakini ina nafasi ya kusonga mbele kama itashinda mechi zake mbili zilizobaki huku ikiomba wapinzani wao Bejaia na Medeama ya Ghana wasipate zaidi ya pointi moja katika mechi mbili walizobakiza.

Katika mchezo wa leo, Pluijm amebadilisha safu ya ulinzi wa kati. Amewaondoa mabeki wake wakongwe, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani huku akiwapa mikoba Mtogo, Vincent Bossou na Andrew Vincent ‘Dante’.
Pia, safu ya ulinzi wa pembeni inatarajiwa kuwa na mabadiliko katika namba tatu iliyokuwa ikichezwa na Oscar Joshua ambayo leo Haji Mwinyi anatarajiwa kuanza. Utakumbuka katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bejaia nchini Algeria, beki huyu alipewa kadi nyekundu.

Post a Comment

 
Top