0



 Mchezaji wa timu ya Hawili fc mwenye jezi nyeupe akijaribu kusambatisha baki ya Kigamboni fc jana katika uwanja wa Halmshauri ya wilaya ya Liwale

Timu ya Hawili fc jana agosti 15 imeweza kulipiza kisasi baada ya uibuka ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kigamboni fc katika ligi ya Alizeti cup iliyomalizika jana katika hatua ya mtoano mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale.

Mabao ya Hawili fc yalifungwa na Faustine Ibrahim namo dakika ya 18 baada ya kupenya ukuta wa mabeki wa Kigamboni fc na kutikisa nyavu na dakika ya 70 Faustune Ibrahim alipachika goli la pili baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Weusi Mbala.

Timu ya Hawili fc imeundwa na wachezaji fanyakazi wa sekta mbalimbali wa Halmashauri ya wilayani hapa.

Mlinda mlango wa Kigamboni fc Mrisho Makarapi alifanya kazi kubwa sana licha ya kurusu mabao 2 yaliyosababisha na  uzembe wa mabaki kurusu kuwapisha wachezaji wa Hawili fc lakini mlinda mlango huyo aliweza kulilinda lango lake vizuri.

 Akizungumza na Liwale Blog kocha wa Hawili fc,Hasani Malapo alisema mechi ilikuwa vizuri na wanajiandaa na mechi ijayo ushindi utategemeana na timu itakuwaje na wao wataikabilialiaje.

Wakati kocha wa Kigamboni fc,Maulidi Masula alisema matokeo ya kuchapwa mabao 2 ameyakubali lakini aliwatupia lawama waamuzi wanaochezesha kuwa hawatoshi.

Ligi ya Alizeti ni maalumu kwa kuhamasisha wakulima wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi walime zao jipya la alizeti.
Timu zilizoingia katika hatua ya robo fainali ni timu ya Polisi fc,Wood pecker,New generation,Sido fc,Hawili fc na Red lion.

Timu ya Red Lion ni Timu ambayo ilipata bahata ya kipee kuingia hatua ya robo fainali baada ya kukosa timu ya kucheza nayo siku ya upangaji wa ratibu kwakuwa timu zilizoshiriki kuwa 13.


Post a Comment

 
Top