Mchezaji ghali
zaidi kununuliwa na Leicester City Ahmed Musa, aliyenunuliwa pauni
milioni 16 na kuvunja rekodi ya klabu hiyo, amewafungia mabao yote
mawili katika mechi ambayo wamefungwa 4-2 na Barcelona katika michuano
ya Kombe la Kimataifa la Klabu.
Munir alifungua ukurasa wa mabao
kupitia pasi iliyotoka kwa Lionel Messi kabla ya nyota huyo wa Argentina
muda mfupi baadaye kumuandalia pasi safi Luis Suarez aliyeongoeza la
pili katika mchezo huo uliochezewa uwanja wa Friends Arena mjini
Stockholm, Sweden.Munir aliongeza la tatu, kabla ya Musa kukomboa bao moja.
Musa alifanikiwa kukomboa la pili lakini nguvu mpya wa Barca Rafa Mujica, mwenye umri wa miaka 17 pekee, akaifungua Barcelona la nne dakika za mwisho mwisho.
"Msimu uliopita Leicester walishangaza sana katika soka ya Ulaya, na hii ndiyo sababu inayomfanya kila mtu kuupenda mchezo huu," meneja wa Barcelona Luis Enrique alisema baadaye.
Upande wa Barca, kando na Messi na Suarez, kulikuwa na nyota wengine kama vile Javier Mascherano na Sergio Busquets.
Leicester wataanza kutetea taji lao la Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City ugenini mnamo tarehe 13 Agosti.
Post a Comment