Takriban 18,000
wamefariki katika jela za serikali nchini Syria tangu kuanza kwa
maandamano dhidi ya serikali mwaka 2011 kulingana na shirika la habari
la Amnesty International.
Ripoti mpya ilioandikwa na shirika hilo
la hisani, lililowahoji waathiriwa 65,inaelezea utumizi wa ubakaji na
kipigo walichopata kutoka kwa walinzi wa jela.
Wafungwa wa zamani
walielezea sherehe za kukaribishwa katika jela kupitia tambiko la
kupigwa kwa kutumia vyuma na nyaya za stima.
Serikali ya Syria kwa mara kadhaa imekana madai hayo.
Ripoti
hiyo inakadiria kwamba takriban watu 17,723 walifariki wakiwa kizuizini
kati ya mwezi Machi mwaka 2011 wakati maandamano hayo dhidi ya rais
Bashar Assad yalipoanza na Disemba 2015 sawa sawa na takriban watu 10
kila siku ama zaidi ya watu 300 kwa mwezi.
Kulingana na ripoti
hiyo ,wafungwa wapya hufanyiwa ukaguzi wa kiuasalama ambao unahusisha
wanawake wanaohusishwa kingono na walinzi wa kiume.
Post a Comment