Katika tweet ya bwana Steve Hemmerstoffer ambaye mwandishi wamtandao wa NowhereElseFr, ambao ni maarufu kwa kuvujisha habari za mkampuni makubwa ametuma pich tatu za matoleo hayo.
Inasemekana iPhone 7 itakuja katika matoleo matatu ya iPhone 7, iPhone 7 Plus na iPhone 7 Pro. Picha kama hizi pia zimeonekana katika mtandao wa kijamii wa China, Weibo. Katika picha hizo, iPhone 7 Pro na iPhone 7 Plus zinaonekana kufanana kimaumbo japo inasemekana iPhone 7 Pro itakuwa na nguvu na vitu vingi zaidi.
iphone 7
Apple inatarajiwa kuachia simu hizo katika mkutano wao wa Septemba
maalumu kwa ajili ya kuachia matoleo mbalimbali ya vifaa vyao. Tetesi
zinasema iPhone 7 itakuja na RAM ya 3GB na kioo cha QHD au 4K na
processor ya hexa-core.
Post a Comment