Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga,
amewasimaisha kazi watumishi sita wa Halmashauri wa halmashauri ya
wilaya ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kutoa taarifa za uongo
kwa kiongozi wa mbio za mwenge.
Watumishi hao ambao wengine ni wakuu wa idara wamesimamishwa kazi baada
ya kubainika kutoa taarifa za uongo kuhusu miradi iliyozinduliwa na
kufunguliwa na mbio za Mwenge mkoani humo.
Wakati wa Mbio za Mwenge Mkoani humo Kiongozi wa Mbio za Mwenge George
Mbijima, alibaini kuwa mradi wa vijana wa Membe kati kuwa ni mradi hewa
huku halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ikitoa hundi hewa kwa
saccos ya vijana ya mjini Kigoma.
Kufuatia matukio hayo ya Uzembe na Udanganyifu ndipo Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma Emanuel Maganga alipochukua hatua ya kuwasimamisha viongozi hao
ambao walisika na udanganyifu huo.
Post a Comment