CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime mkoani Mara kimewaonya vijana
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaodai kuwa watakwenda
Dodoma kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM mwishoni mwa
wiki hii, wasithubutu kufanya hivyo.
Aidha, uongozi na wanachama zaidi ya 2,000 wa CCM wilayani hapa, wamempongeza Rais John Magufuli kwa uteuzi wa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi watendaji wa miji, manispaa na wilaya alioufanya hivi karibuni.
Onyo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya, Rashid Bogomba wakati wa kikao cha chama hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki wilayani humu.
Alisema, “Tunawaonya vijana wa Chadema (Bavicha) waliotangaza kwenda Dodoma kuvuruga mkutano maalumu wa CCM kwa sababu ni halali na uko kwa mujibu wa katiba. Pia tunapinga na kukemea vitendo haramu vyote vinavyofanywa na vijana hao,” Aliongeza kuwa, mikutano iliyopigwa marufuku ni ya siasa ya hadhara na si vikao kama hivyo, kwa sababu hata Chama cha Wananchi (CUF) kinategemea kufanya mkutano wake wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama hicho Agosti mwaka huu na ni kikao halali cha kikatiba.
Katika hatua nyingine, alimpongeza Rais John Magufuli kwa uteuzi alioufanya hivi karibuni wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Miji.
Alisema kuwa wako tayari kushirikiana nao kuhakikisha wanafanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM yenye lengo la kuhakikisha maendeleo ya nchi. “Tunawaomba Watanzania wenzetu kumuunga mkono Rais wetu Magufuli katika juhudi zake za kupambana na ufisadi na maovu hapa nchini.

Post a Comment