WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Angella Kairuki, amesema Serikali ya Awamu ya Tano italipa
madeni ya wazabuni na ya watumishi wa serikali bila matatizo baada ya
kuhakikiwa na kujiridhisha.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa umma kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Hatua hiyo ilitokana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe kumfahamisha waziri kuwa mkoa huo unadaiwa madeni yenye kufikia kiasi cha Sh bilioni 1.1 kutoka kwa wazabuni pamoja na ya watumishi wa umma, wakiwemo walimu.
Kairuki alisema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kulipa madeni ya watumishi na wazabuni baada ya kukamilisha uhakiki wa madeni hayo utakapofanyika ili kupata deni halali. “Uhakiki wa madeni unafanyika na deni halali litalipwa bila tatizo,” alisema Kairuki.
Awali, Dk Kebwe alisema fedha zaidi ya Sh bilioni 1.1 zinahitajika kwa ajili ya kulipa madeni ya aina mbalimbali ambayo ni pamoja na wazabuni wa hospitali ya mkoa na shule za sekondari za bweni za serikali, ikiwa na watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo walimu.
“Kiasi hiki cha fedha zaidi ya shilingi milioni 800 ni madai ya watumishi wa kada mbalimbali kutoka halmashauri za mkoa, wakiwemo na walimu, kingine zaidi ya milioni 300 ni deni litokanalo na wazabuni,” alifafanua Dk Kebwe.
Naye Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa (Mipango), Diaz Ndomba alisema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika dirisha la malipo la mwezi Mei na Juni mwaka huu kilipokewa kiasi cha Sh 1,942,474,500 kwa ajili ya malipo kwa kaya 50,678 zilizomo kwenye Mpango wa kunusuru kaya maskini katika halmashauri saba za mkoa huo.
Ndomba alizitaja halmashauri hizo ni Manispaa ya Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Gairo, Kilosa, Mvomero, Ulanga na Kilombero, wakati halmashauri mpya ya Malinyi na ya Ifakara Mji hazijaingizwa katika utekelezaji wa mpango huo.

Post a Comment