0

Wanafunzi zaidi ya 220, hawajapata  stahidi zao. Teofilo Kisanji University (TEKU) campus ya Mbeya,zaidi ya wanafunzi 220 wa course tofauti tofauti hawajapata pesa zao za field( mafunzo kwa vitendo) na special faculty, toka tar 4/4/ 2016 adi tar 15/ 5/2016 chuo kiliwapeleka wanafunzi kuenda kufanya field,  hasa wanafunzi wa mwaka wa pili na wa kwanza.

Utaratibu ni kwamba hawa wanafunzi wanasomeshwa na serikali kwa hiyo huchukuwa dhamana ya kuwapa pesa ya kujikimu kila mmoja kiasi cha Tsh 10000 kwa siku pamoja na 60000  kwa ajili ya usafiri hivyo basi kufanya jumala ya 480000 kila mmoja, kwamaana hiyo pesa ambayo hawajaweza kupata kwa idadi hiyo kufanya Tsh,  105.6million.

Wanafunzi hao hao hawajapata pesa zingine za special faculty, kila mmoja alitakiwa kupata 60000 kwa mwaka kufanya jumla ya Tsh 13.2 million, tatizo lilianza kama ifuatavyo, toka sheet ya majina ya kusain zaidi ya idadi hapo juu 220 hayakuoneka kwenye hiyo sheet. Hivyo tulijaribu kufuatilia juhidi zetu apa chuoni hazijaa zaa matunda tukaona hiyo haitoshi tukamtuma mwenzetu loan board
( HESLB) hakuja zaa matunda, maasikini tumekosa nini wanafunzi sisi.

Ukiangalia tunaishi maisha magumu adi leo hatuna ata senti ya kuweza kujikimu,  ombi letu, tunaomba msaada ya dharura kuweza kunusulu maiasha yetu, tunaamini kupitia serikali makini na sikivu chini ya Dr. John Pombe Magufuri. Kupitia wizara yenye dhamana na masuala ya Elimu, hasa wizara ya Elimu Sanyansi na Technologia kuweza kutusaidia juu ya mkwamo huu,

source mwanafunzi

Post a Comment

 
Top