UMOJA wa walimu, wanafunzi na wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu
jijini Dar es Salaam, umekemea vitendo vya rushwa ya ngono vyuoni kwamba
vinadhalilisha, kunyanyasa na kumuondolea binadamu heshima yake.
Walisema pia kuwa waathirika wa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono, wanaathirika kisaikolojia.
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa Umoja wa kupambana na rushwa ya ngono vyuoni ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Colman Msoka baada ya semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia (GTI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Women Fund Tanzania.
Alisema kuwa rushwa ya ngono imekuwa ikisababisha magonjwa, vifo, mfarakano na kulipiziana kisasi.
Dk Msoka alisema kuwa vitendo hivyo pia vinasababisha watumishi hewa, wataalamu wabovu, utendaji kazi duni, nidhamu mbovu miongoni mwa wanafunzi, waajiri, walimu, wanafunzi na makundi mengine.
“Kushamiri kwa vitendo hivi vya rushwa ya ngono kunatokana na imani iliyopo kwa baadhi ya wanawake na wanaume kuwa na mafanikio yao yatapatikana kwa urahisi zaidi kwa kutoa rushwa ya ngono. Mafanikio hayo ni pamoja na kupata kazi, elimu, kufaulu mitihani au kupata fursa nyinginezo,’’alisema.

Post a Comment