Vodacom
imekuwa na dhamira ya kufanya ubunifu wa teknolojia kwa ajili ya
kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa
kuwapatia huduma bora za kurahisishia maisha na kwa gharama nafuu.
Sasa good
news ni kwamba leo kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imezindua ofa mpya
maalum kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Ya kwako tu’
itakayowawezesha kujipatia vifurushi vya ghrama nafuu kwa kadri ya
matakwa yao wapendayo kuanzia vya huduma ya kuperuzi internet ‘mitandao
ya kijamii, youtube, whatsapp na kadhalika’, kupiga simu ‘kwenda
mitandao yoyote na kutuma ujumbe mfupi wa maneno.
Ili uweze kujiunga na huduma hiyo unatakiwa kupiga namba*149* 03# na kuchagua ofa ya kwako.
Mkurugenzi
wa mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia
(katikati), kushoto ni Afisa Mkuu wa Idara ya masoko wa kampuni hiyo,
Ashutosh Tiwary na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa kampuni hiyo,
Danilo De Sousa.
Post a Comment