Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha magari
matatu likiwemo basi mali ya kampuni ya Ota iliyotokea katika eneo la
Veta Dakawa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imeongezeka hadi kufikia
vifo 12 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa na hali mbaya kufariki dunia
wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na ITV kwa njia ya simu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mtakatifu Joseph iliyopo Dumila Suleman Senkoro amesema majeruhi wote wamepata nafuu na kuruhusiwa huku Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Morogoro Frances Semwene amethibitisha kupokea majeruhi 8 huku kati yao mmoja akifariki wakati akipatiwa matibabu.
Kwa upande wao majeruhi wa ajali hiyo wesema wanaendelea vizuri ambapo wametupia lawama wamiliki wa mabasi kuwatelekeza wanapo pata ajali pamoja na kulalamikia ukosefu wa dawa katika hospitali hiyo ambapo wameiomba serikali kuona jinsi ya kuiwezesha hospitali hiyo ilikuweza kumudu matibabu inapo tokea majanga ya ajali.
Ulrich Matei ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ambapo ameiambia ITV jeshi hilo linamtafuta dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo na kutoweka kusikojulikana huku akiwataka madereva kutii sheria za barabarani.
Miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro imeendelea kuchukuliwa na ndugu zao hadi sasa umebaki mwili mmoja ambao bado ndugu hawajafika.

Post a Comment