0



Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam ametoa msaada wa vyakula na bidhaa mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto hao cha Shinyanga Society For Orphans kilichopo mtaa wa Viwandani mjini Shinyanga.



Akizungumza leo wakati wa kukabidhi msaada huo wa chakula na vifaa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili,Mukadam ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti wa majiji,manispaa na halmashauri zote nchini Tanzania (ALAT),alisema chakula hicho kitawasaidia watoto hao katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani,Siku ya Sikukuu ya Idd El Fitri na vitakavyobaki wataendelea kuvitumia katika kituo hicho.



“Nilipewa taarifa kuwa kituo hiki kinahitaji msaada,ndiyo maana nimeona nijibane bane kusaidia watoto hawa,wengine wamefunga katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani,tunaungana nao katika funga hii,nimewaletea chakula kwa ajili ya Futari na Daku”,alisema Mukadam.


“Chakula na bidhaa zote hivi zimegharimu takribani shilingi milioni moja na laki mbili,watoto hawa ni wetu sote..mimi kama sehemu ya jamii nimeona vyema kutoa msaada huu walau uwasaidie katika kipindi hiki wakiwa wamefunga,wakati wa sikukuu na baada ya sikukuu kwani naamini chakula na bidhaa vitabaki baada ya sikukuu na wataendelea kuvitumia.


Mukadam ambaye pia ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini pia mwenyekiti wa wenyeviti wa majiji,manispaa na halmashauri zote nchini Tanzania (ALAT),alivitaja vitu alivyotoa kwa watoto hao kuwa ni Unga sembe kilo 75,Mafuta ya kupikia lita 60 na Unga wa ngano kilo 75.


Vingine ni Sukari kilo 75,chumvi kilo 70,sabuni za kufulia katoni 3,sabuni ya unga mifuko 2,blue band makopo 3,biskuti katoni 3,mafuta makubwa ya kujipaka dazani 1,mchele kilo 150,sabuni za kuogea dazani 3 na nyama kilo 30.


Pia kuna soda katoni 10,juisi katoni 4,ndizi matoke mikungu 3,viazi ulaya kilo 30,maharage kilo 30,tambi kilo 60 na tende katoni 3.


Akipokea msaada huo Baba mlezi wa kituo hicho cha watoto yatima Said Sakala alishukuru kupata msaada huo na kuomba wadau wengine wa maendeleo katika jamii kujitokeza kusaidia watoto na vikundi mbalimbali vyenye mahitaji. 

Geti la kituo hicho

Vyakula vilivyotolewa na mheshimiwa meya Gulam Hafeez Mukadam


Unga wa ngano






Meya manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akiwa na baba mlezi wa watoto hao Said Sakala





Baadhi ya watoto waliofunga katika kituo hicho



Post a Comment

 
Top