Waziri wa fedha wa
Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake yenye lengo la
kupunguza kodi muhimu ya faida katika biashara.
Hatua ya Osborne
ni sehemu ya mkakati wa kiuchumi katika harakati za kuvutia uwekezaji
mpya, na hii inafuatia kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo
iliamua Uingereza isite kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya.Osborne aliliambia gazeti la Financial Times kwamba anataka kupunguza kodi ya shirikishi kutoka asilimia ishirini hadi chini ya asilimia kumi na tano.mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara ameeleza kwamba kura ya maoni ilikuwa ni mkakati wa kuisaidia Uingereza kuvutia uwekezaji kutoka kwa kampuni mbali mbali mpango ambao inawezekana haukufanikiwa kufuatia kura hiyo ya maoni
Post a Comment