0

Mchazaji wa timu ya Nangando fc akiwa katika harakati ya kugawa basi 


Robo fainali ya 3 ya Lig ya Liwale Super cup leo iliendelea kutimua vumbi uwanja wa wilaya ya Liwale  kulikuwa na timu ya Transpoter fc Vs Nangando fc. 

Transporter fc iliweza funga dakika ya 3 na Abuu Kazumali na Nangando fc iliweza kusawazisha  goli dakika ya 39 lilofungwa na Imamu Katundu. 

Katika kipindi cha pili Transporter fc iliongeza goli katika dakika ya 55 lilofungwa na Saidi Milasi. 

Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa Transporter 2-1 Nangando fc. 

Transporter fc imeweza kuingia nusu fainali
Kesho kutakuwa na mchezo uingine wa robo fainali kati ya Sido fc Vs Polisi Fc

Post a Comment

 
Top