Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John ambaye amepandikizwa betri ya umeme wa moyo kwenye mfumo wa moyo wake.
Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri.
Dk Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa Peacemaker (Betri ya umeme wa moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa binadamu.
Aidha amesema upasuaji huo ni wa kwanza kufanyika nchini ambapo upasuaji kama huo unafanyika kwa watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa kupandikiza na kwamba tatizo la mtoto huyo ni la kuzaliwa ambalo ni nadra kutokea.
Mama wa mtoto huyo, Elitruda Malley ambaye ametokea mkoani Arusha amewashukuru madaktari wa taasisi hiyo kwa kufanya upasuaji huo na mtoto wake kutoka salama katika chumba cha upasuaji.
Post a Comment