BAADA ya kuenea taarifa za mshambuliaji, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji kuwa yupo mbioni kutua AS Roma ya Italia, Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo amekanusha kwa kusema ni uzushi mtupu.
Taarifa hiyo jana asubuhi, ilienea katika mitandao ya kijamii ikieleza kuwa AS Roma ipo kwenye mazungumzo Genk ya kumchukua mchezaji huyo na leo alihitajika kwenda nchini Italia kuzungumzia dili hilo.
Akizungumza na , Kisongo alisema kuwa hakuna uhusiano wowote wa Samatta kutua katika miamba hiyo ya Italia kutokana mchezaji huyo anamkataba wa muda mrefu.
Alisema kwa sasa Samatta anaendelea na maandalizi ya msimu mpya na mechi zao za mtoano wa Ligi ya Uropa ambazo zitachezwa mwezi ujao katika timu yake hiyo ya Genk.
“Hakuna jambo lolote kuhusiana na Samatta kwenda AS Roma, hizo ni habari za kizushi na hazina ukweli wowote kwani tunaheshimu mkataba wa sasa alionao mchezaji wangu, lakini kama kuna klabu itakuja nitakuambia juu ya hilo," alisema Kisongo.
Alisema amekuwa akizisikia taarifa hizo kupitia katika mitandao ya kijamii na kupigiwa simu na rafiki zake pamoja watu mbalimbali ambao ni wadau wa mpira wakiulizia hilo.
Mwandishi wetu limtafuta Samatta mwenyewe alisema kuwa hana taarifa hizo licha kuona zinakuzwa kwa kasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii lakini kama ikiwa kweli ni jambo la kheri.
"Sina taarifa hizo naziona zinasambaa kwa kasi kubwa, ila kama itakuwa kweli siwezi kukataa dili kama hilo kutokana mpira ni kazi yangu," alisema.
Post a Comment