0
                            Mchezaji wa timu ya Sido fc akionesha ufundi uwanjani
              Mchezaji wa timu ya Mpengele fc akionesha ufundi uwanjani lakini haraki zilishindikana

Makocha wa timu ya Sido fc Mohamedi Hema (kushoto) walifuatilia kwa makini wachezaji wao ili kuhakikisha wanashinda




Mchezaji wa timu ya Sido fc akipewa msaada wa huduma ya kwanza mara baada ya kuchezewa vibaya
                                Mlinda mlango wa timu ya Mpengele fc
             Goli la pili lililofungwa na Hamza Lipupu dakika za lala salama dakika ya 85
                        Zawadi za washindi wa ligi ya Liwale Super Cup
Picha ya pamoja kati ya timu ya Mpengele fc na moja ya mshabiki wa timu ya sido fc mwenye singelindi nyekundu
Katibu wa chama cha mpira wilaya ya Liwale Nurdin Kazumali (kushoto) akikabizi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa pili kwa kapteni wa timu ya Mpengele fc
Katibu wa chama cha mpira wilaya ya Liwale Nurdin Kazumali (kushoto) akikabizi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa pili kwa kapteni wa timu ya Mpengele fc
Kapteni wa timu ya Sido fc Haikosi Mpwate kakitoa neno kabla ya kukabiziwa kombe
Mabingwa wapya wa Liwale Super Cup ambao ni timu ya Sido fc wakikabiziwa Ng'ombe mara baada ya kuibuka washindi baada ya kuilaza Mpengele fc mabao 2-1
Mabingwa wapya wa Liwale Super Cup ambao ni timu ya Sido fc wakikabiziwa Ng'ombe mara baada ya kuibuka washindi baada ya kuilaza Mpengele fc mabao 2-1
 Timu ya Sido FC imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Liwale Supercup baada ya kuikung'uta Mpengele FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Halmashauri ya wilaya Liwale.

 Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa kila timu ilionekana kuwa na shauku ya kupata bao. Sido ilianza kufungua kalamu ya mabao baada ya kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Hamza Kilemba dakika ya 10 na bao la pili lilifungwa na Hamza Lipupu dakika ya 85.

 Katika mchezo huo Mpengele walipata penaiti ilipigwa na mchezaji Jabiri Likana lakini alikosa kufunga baada ya mpira kupiga nje ya goli. Mchezo uliendelea kuchezwa kwa kasi kwa kila timu ikisaka magoli lakini namo dakika ya 85 Hamza Lipupu aliweza kuiandikia Sido fc goli la pili na goli hilo lilidumu mpaka dakika 90 zinakamilika.

 Zawaidi zilizotolewa kwa washindi leo ilikuwa kama ifuatavy,Timu ya Sido fc ambao ndio mabingwa wa ligi ya Liwale super cup waliweza kupewa Ng'ombe na washindi wa pili ambao Mpengele fc waliweza kuzawadiwa Mbuzi. 

Baada ya kumalizika mchezo makocha waliweza kuongea na Liwale Blog kuzungumzia mchezo wa leo kwa upande wa kocha wa Sido fc Mohamedi Hema alisema mchezo ulikuwa mgumu toka dakika za mwanzo pia aliweza kubainisha siri ya ushindi kwa timu yake.

 "Nilijiandaa vizuri toka mwanzo wa ligi na kikubwa kilichonisaidia ni umoja na ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wakati wote wa mazoezi mpaka siku ya mechi' alisema Mohamedi Hema 

Kocha wa timu ya Mpengele fc Twalibu Matengana alisema mchezo wa leo ulikuwa mgumu kwa pande zote makosa yaliofanywa na timu yake ndio waliweza kutimia wapinzani wao na kuweza kufunga na amekili matokeo ya mchezo wa leo lakini aliweza kutoa mapendekezo kwa upande wa waamuzi wa ligi kwa kusema zilijitokeza kasoro ndogondogo na kuomba uongozi wa soka wilayani kuzishughulikia ili kuweza kuboresha na timu nyingi kuweza kushiriki ligi mbalimbali na watu kuweza kuonesha vipaji vyao.

Post a Comment

 
Top