0
 
Fernandez anadaiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi
Polisi nchini Argentina wanasaka mali za Rais wa zamani wa nchi hiyo Cristina Fernandez de Kirchner.
Upekuzi unafanyika katika jimbo la kusini la Santa Cruz,kwa amri ya mahakama.
Fernandez anadaiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini humo.
Hii ni kwa mara ya pili familia ya Rais huyo wa zamani kuvamiwa kwa sababu hiyo.
Mwaka jana Hoteli pamoja na baadhi ya majengo yalifanyiwa upelelezi mkali na wana usalama wa nchi hiyo.
Fernandez anamtuhumu Rais wa sasa Mauricio Macri kuwa anafanya mchezo mchafu wa kisiasa juu yake.

Post a Comment

 
Top