MADIWANI wawili wameunganishwa katika kesi ya kumjeruhi Katibu Tawala wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando inayowakabili watu sita wakiwemo
wabunge watatu wa Chadema.
Madiwani waliounganishwa katika kesi hiyo na kusomewa mashtaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi, ni Diwani wa Kata ya Liwiti, Edwin Mwaipaya na wa Segerea, Edwin Mwakatobe.
Wabunge wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga) na Saed Kubenea (Ubungo). Madiwani wengine ni Ephrein Kinyafu (Kimara), Manase Njema (Tabata Kimanga) na kada wa chama hicho, Rafii Juma.
Awali Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson alidai kesi hiyo imetajwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali kabla ya kuomba washtakiwa wengine waunganishwe.
Mahakama ilikubaliana ombi hilo. Esterzia alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama ya kutenda kosa la jinai na kujeruhi Februari 27, mwaka huu kwenye uchaguzi wa meya na naibu meya wa jiji la Dar es Salaaam, uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Washtakiwa walikana mashtaka yao na kuachiwa kwa dhamana baada ya kujidhamini. Wakili wa utetezi, Fredrick Kihwelo alidai mahakamani kuwa Mdee amekwenda Canada kikazi na Waitara anaumwa, ndiyo maana wameshindwa kufika mahakamani.
Hakimu Shahidi alisema sababu zote zilizotolewa hazina msingi, kwa sababu Waitara anaumwa lakini Mahakama haijapokea cheti. Alisema Mdee amekwenda Canada kwa shughuli zake binafsi na kuwataka waheshimu taratibu na sheria zilizowekwa. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 27 mwaka huu.

Post a Comment