0



TAARIFA KWA UMMA.

Tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa, Sisi Madiwani wa CHADEMA Manispaa ya Shinyanga, tuliamua kutoka nje ya ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Madiwani la Mwaka, lililoketi Ijumaa tarehe 29, mwaka huu katika Ukumbi wa Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kutokana na sababu mbalimbali.

Kwamba, Naibu Meya Bibi Agnes Machiya, (Diwani kata Kolandoto) kwa MAKUSUDI KABISA ya kutaka Kujilinda na Kulinda Ufisadi na Mchafu mkubwa katika manispaa yetu, aliamua kuvunja kanunu za kudumu za Halmashauri ya Manispaa Shinyanga za mwaka 2013.

Ifahamike kuwa, Kwa mujibu wa Kanuni ya 27, ya Kanuni za kudumu za Halmashauri, inatamka Mchangiaji kuwa na Uhuru wa kutoa Mawazo. Kanuni inasema... "Kutakuwa na uhuru wa kutoa mawazo wakati wa majadiliano katika mikutano ya Halmashauri na uhuru huo hautaweza kuhojiwa katika MAHAKAMA yeyote ana MAHALI popote nje ya Mkutano wa Halmashauri"

Katika Baraza hilo tulizuiliwa kuhoji juu ya ufisadi wa Mamilioni ya ununuzi wa Mtambo wa Greda, lenye thamani ya Fedha za Kitanzania zaidi ya milioni Mia Tano TZS 500,000,000. Eti kwa kisingizio kwamba, swala hilo lipo TAKUKURU.

Tunaamini msingi wa zuio hilo la Naibu Meya ni kuta kulinda kashfa ya Ufisadi wa ununuzi wa Greda hilo unaomkabili Meya na Mkurugenzi wa kipindi hicho. Ambao walikwenda Dar es salam na kufanya manunuzi kinyume cha Sheria ya manunuzi ya mwaka 2010.

Kwa mujibu wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikari(CAG) Greda hilo halijawahi kufanya kazi kwa kiwango toka linunuliwe mapema mwaka 2015. Kwamba ni bovu na halifai.

Msimamo wetu: Greda hilo lirudishwe kwa mzabuni huyo Muhindi wa Kampuni ya GF TRUCK & EQUIPMENT LTD na Wahusika wote wachukuliwe hatua kali za kimaadili na kisheria, na kwamba Kinyume cha hapo PATACHIMBIKA..

Aidha, Naibu Meya aliamua kutuziba midomo ( kwa kutukatisha kuongea) kwa kuwa kulikuwa na Hoja ya Kimaadili ya kuhusu ufisadi wa Mfuko wa Jimbo, ambapo yeye mwenyewe Naibu Meya ni Mtuhumiwa katika -Kamati ya Maadili- pamoja na Mbunge, kwa pamoja walivunja Sheria ya Mfuko Maendeleo wa Jimbo ya Mwaka 2009.

Pamoja na hayo Naibu Meya aliamua kutuziba midomo kwa kuwa, kulikuwa na hoja ya kwanini Mwanasheria wa Manispaa analipwa POSHO YA MOTISHA Shilingi Milioni Mbili kisa kashinda kesi? Tunahoji vipi kuhusu Kesi alizoshindwa anailipa Halmashauri? Malipo hayo wanalipa kwa kuzingatia sheria na kanuni ipi?.

Vilevile Naibu Meya aliamua kutuziba midomo kwa kuwa, Kulikuwa na hoja juu ya Tenda ya Kampuni ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Kuhoji ni kwanini kampuni hiyo imepewa muda mrefu sana wa siku 120 yaana miazi minne. Kukwangua barabara yaana (Routen Maintenence) Miezi4? Kukwangua? Wakati wakandarasi wengine wenye kazi kama hiyo (RM) wakipewa miezi miwili yaan Siku60.

Ifahamike pia, naibu meya alishindwa kujibu hoja ya kutaka kufanyika Uchanguzi wa Naibu Meya kulingana na kanuni ya 41 (5) inasema kila Mkutano wa Mwaka wa Halmashauri huchaguliwa wajumbe wapya.

Mwisho Naibu Meya alihamaki, hakuzingatia Kanuni na Kutoa Upendeleo wa kuzungumza kwa muda mrefu Wajumbe wa CCM na kutunyima fursa hiyo Madiwani wa CHADEMA, kutokana na maswala tajwa hapo juu. Kwa busara tukaona ni vema tutoke nje kwa kuwa Bibi alikosa mwelekeo.

NB: Ikumbukwe kuwa hata kwenye Baraza la Tarehe 07-04-2016, Tuliwapisha Madiwani wa CCM wakapitisha azimio la kuruhusu NGO ya RAFIKI kusambaza mafuta ya Vilainishi Shinyanga CHADEMA, Tulipinga na sasa Serikali kuu ya CCM inapinga Azimio la Baraza la Madiwani wa CCM

Tunasema, "Hakuna kulala mpaka Mafisadi wa Greda washugulikiwe"

"Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke...Viva UKUTA viva UKUTA.

Wasalaam,

Emmanuel Ntobi
Mwenyekiti Madiwani CHADEMA Manispaa Shinyanga.

Post a Comment

 
Top