Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe
inawashikilia watumishi wake wawili wa wilaya ya Makete kwa tuhuma za kuomba
rushwa ya shilingi laki sita kwa mwananchi jina lake
limehifadhiwa kwa usalama wake ambaye alikuwa anakabiliwa na tuhuma za
kugushi vyeti vya ajira wilayani humo.
Kamanda wa TAKUKURU
mkoa wa Njombe Charles Nakembetwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja
na mwanasheria wa taasisi ya TAKUKURU wilaya ya Makete Frednand Nsakuzi
pamoja na mlinzi wa ofisi ya TAKUKURU Makete Julius Hassan
wote watumishi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilani Makete.
Amesema watuhumiwa
hao kwa pamoja waliomba kiasi hicho cha fedha shilingi laki sita
kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa June 28 mwaka
huu majira ya saa moja na saa mbili usiku ambapo waliomba
rushwa kwa mwananchi huyo aliyekuwa anatuhumiwa kugushi vyeti vya
ajira.
Nakembetwa amesema watuhumiwa
hao walifanikiwa kupokea fedha ya awali shilingi laki moja
ambapo baada ya TAKUKURU mkoa wa Njombe kupata taarifa hizo
walifanikiwa kuweka mtego ulio wanasa watuhumiwa hao.
Amesema walifanikiwa
kuwakamata wahusika wakiwa wanachukua fedha hizo kinyume na
kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba
11 ya mwaka 2007.
Post a Comment