0



Mahakama ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 katibu wa mkuu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya kusini kati Edward Ahazi Masevele kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ubakaji na udharirishaji kwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa la tano wilayani humo.



Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo kwa muda wa miaka miwili, ambalo linaambatana na mashtaka ya kumjeruhi mwanafunzi huyo kwa kutumia vidole vyake kumjeruhi sehemu za siri kabla ya kufanya vitendo vya ngono jambo ambalo ni ukiukwaji wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009, Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 ni waraka unaoshughulikia masuala mengi ya kitaifa yanayohusu haki na ulinzi wa mtoto.


Sheria hii pia imechukua mikataba na makubaliano mbalimbali ya kimataifa yanayohusu haki za mtoto, na vilevile kutoka kwenye sera ya taifa ya watoto inaweka bayana muundo unaolenga kumpa mtoto kinga pamoja na viwango kwa ajili ya utoaji haki kwa watoto katika sheria hii mpya Na. 21 ya mwaka 2009.


Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Njombe Cosmas Joseeph Hemela alisema kwa kuzingatia kifungu cha sheria namba 130 (1 na kifungu cha 131 ,1) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 mahakama hiyo imemkuta na hatia Masevele kwa kosa la ubakaji na udharirishaji wa mtoto.


Kosa la pili ni shambulio la aibu kwa kumwingiza vidole mtoto huyo sehemu za siri kwa kuzingatia kifungu cha sheria namba 138 (1 a) na 2 b kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo katika kipengele hicho kosa hilo adhabu ya miaka miwili.



Kutokana na kipengele hicho, mahakama imemtia hatiani baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka dhidi ya mtuhumiwa ambaye alifanya kosa hilo na rufani ipo wazi kwa mtuhumiwa ndani ya siku 30.


Mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya mwaka 2015 hadi aprili mwaka 2016 na kufikishwa mahakamani mnamo Mei 10 mwaka 2016 ilipotajwa kwa mara ya kwanza.

Chanzo:Malunde1 blog Njombe

Post a Comment

 
Top