Mbunge wa jimbo la Liwale,Mh.Zuberi Kuchauka akiongea na wananchi wake katika mkutano wa hadhala uliofanyika jana katika uwanja wa Nanjinji uliopo kijiji cha Likongowele kata ya Likongowele Liwale mjini
wananchi wa jimbo la Liwale wakiwa wakiwa kw enye mkutano wa mbunge wao uliofanyika jana katika uwanja wa Nanjinji
Mbunge akinukuu maswali mbalimabili ya wananchi waliouliza ili kupatiwa majibu Mwenyekiti wa chama cha walemavu wilayani Liwale,Bwana Mshamu Mulue akiuliza swali
Bwana Hasani Makuche mmoja ya wananchi waliopata nafasi ya uliza swali hapo jana
Imani Mtesa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Liwale kupitia ACT nae alipata nafasi ya kuuliza swali kwa mbunge wake
Bi. Somoe Kujakila aliweza kupata nafasi ya kuuliza swali lilohusu mambo ya huduma ya afya katika hospitali ya wilaya wa Liwale
Mohamedi Ngotwike nae aliweza kupata nafasi ya kuuliza swali juu ya majibu ya serikali aliyopewa mbunge wake baada ya mbunge Kuchauka kuuliza maswali mbalimbali akiwa bungeni
Othumani Mkomba aliweza kupata nafasi ya kuuliza swali kwenye mkutano huo wa hadhala
Mshamu Tewele aliweza kupata nafasi ya kuuliza swali kwenye mkutano huo wa hadhala
Mbunge wa Jimbo la Liwale,mh Zuberi
Kuchauka (Cuf) amewata vijana kuchangamkieni fursa zilizopo wilayani hapa ili
kuweza kujikwamu na umasikini.
Hayo aliyasema Jana kwenye mkutano wa
adhara uliofanyika katika uwanja wa mkutano wa Nanjinji katika kijiji cha
Likongowele kata ya Likongowele wilayani Liwale mkoani Lindi.
Kuchauka alisema wilaya ya Liwale kuna fursa
nyingi sana lakini utambuzi wa fursa zilizopo ni mdogo hivyo kinachotakiwa
vijana kuwa tayari kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiliamali ili kuweza
kuchangamkia fursa zilizopo alizitaja baadhi ya fursa zinazopatikana wilayani
hapa kama vile ufugaji wa kisasa wa nyuki,ufugaji na kilimo na aliongeza kusema
serikali ya awamu ya tano alihadi kutoa fedha kila kijiji shilingi milioni 50
hivyo pesa hizo zitagawiwa kwenye vikundi za ujasiliamali.
Pia Kuchauka aliwata wananchi kuwatumia vema
maafisa ugani waliopo katika shughuli zao mbalimbali za kimaendeleo kama
kilimo,ufugaji wa kuku na wanyama na ufugaji wa nyuki ili kuweza kuongeza kipata.
"Ni ajabu sana kuona maafisa ugani na
mifugo wapo hapa wilayani lakini hatuwatumii alafu wanachukua mishahara na
ajabu kuona afisa ugani hana shamba la mfano na hawawatembelei wakulima kwenye
mambasha yenu"alisema Kuchauka.
Kuchauka aliweza kubainisha suala la
fidia kwa wananchi ambao mazao yao yakishambuliwa na wanyapori alisema tatizo kubwa la wananchi
hawafahamu sheria ya jinsi ya kudai na kupata fidia zao lakini serikali
inafahamu na kuna kiwango maalumu kwa kila hekta na umbali wa kutoka shamba
mpaka hifadhi sasa kinachotakiwa mkulima anatakiwa atoe taarifa kwa mtendaji wa
kijiji ndipo hizo taarifa kufikishwa sehemu husika.
Bi Somoe Kujakila aliweza kuuliza
swali kwa mbunge kuna kero sana kwa akinamama wajawazito wakati wa kujifunguo katika
hospitali ya wilaya na dawa hakuna ,Kuchauka alijibu kwa kusema kuwa kero hiyo naifahamu sana na moja ya hotuba
yake ya kwanza bungeni aliongelea kero hiyo ana alisema wilaya ya Liwale haina
hospitali ya wilaya bali kuna kituo tu cha Afya na ameomba akinamama waendelee
kuvumilia na kusema wahudumu wa afya waliopo ni wachache sana na kusema bajeti
hii ikisaidia inaweza kupunguza kero hiyo.
Mohamedi Ngotwike nae alipata nafasi
ya kuuliza swali kwanza nakupongeza kwa harakati zako ulipokuwa unachangia sana
na unauliza maswali bungeni lakini hatujapata majibu ya maswali uliokuwa
unayauliza Kuchauka alisema majibu ya mawaziri yapo kwenye vitabu ambazo
waligawiwa hivyo anaandaa utaratibu wa kuweka kituo binafsi ili kuwapa wananchi
vitabu ili waweze kusoma na kufahamu mambo mbalimbali pia aliongeza kusema
wanaliwale waanzishe utaratibu wa kuanzisha kituo cha sheria ili kuweza kuwapa
msaada wa kisheria wananchi.
Post a Comment