0

Mbunge wa jimbo la Liwale mh.Zuberi Kuchauka akikabidhi mpira kwa kiongozi wa timu ya Mbuli na Nyela katika kata ya Kichinda


MBUNGE wa Liwale Zubeir Kuchauka (CUF) amewataka vijana kujihusisha na michezo wilayani hapa kwa kuwa inatoa fursa kwenye ajira na kujenga afya ya mwili.
 Kuchauka alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Mbuli na Nyela vilivyoko kata ya Kichonda.

  Akiwa katika kijiji cha Nyeli na Mbuli  alikabidhi mpira kwa vijana ambao walimwelezea mbunge huyo adhma yao ya kuwa na michezo lakini wanakabiliwa na ukosefu wa vifaa.

  Kijana Fadhili Mwekea alimweleza mbunge kuwa wanapenda michezo lakini wanakabiliwa na uhaba wa vifaa ikiwa ni pamoja na mpira kwani wanafuma mipira ya makaratasi ambayo haikai kwa muda mrefu huku wakiwa na timu ya kijijini hapo.
 
 Mbunge mara baada ya kugawa mipira aliwaeleza vijana hao wajiandae vyema kwani Kombe la Kuchauka liko mbino kuanza na zawadi nono zitatolewa kwao.

  Alizitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na mshindi wa kwanza laki tano jezi na kombe ,wa pili laki tatu na jezi na wa tatu laki 2 na jezi.

  Alisema atahakikisha michezo Lilwale inapewa kipaumbele na si kwa wanaume tu bali hata kwa wanawake pia.

    Alisema kombe hilo linatarajiwa kusakatwa mnamomwezi Disemba mwaka huu.

Post a Comment

 
Top