Kijana EmanueL Fedrick (20) wenye tatizo la akili akiwa amepaktwa na shangazi yake Stella John mara baada kumaliza kupatiwa chakula. |
Na EmanuelMadafa,JamiiMojablog- Mbeya
JESHI
la Polisi kupitia dawati la jinsia na watoto linamshikilia Baba mzazi
wa kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili ,Emanuel Fedrick
iambaye alifungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake.
Kijana
huyo, mwenye umri wa miaka 20, Fredrick Emmanuel Mkazi wa Mwambeja
Kata ya Iganjo jijini hapa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje
kwa kipindi cha miaka 11, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa
kudhohofisha mwili wa kijana huyo kiafya.
Tukio
la kukamatwa kwa mzazi huyo limetokea Julai 14 ,2015 majira ya asubuhi
nyumbani kwakwe katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi lililopo Jijini
hapa.
Akizungumzia
hilo, Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Mbeya, Afisa wa Polisi Janet
Masangano, amesema baba mzazi wa kijana huyo Emmanuel John, anashikiliwa
na polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia tuhuma zinazomkabili za
kumficha mtoto ndani kwa zaidi ya miaka 11 hali ambayo imetafsiliwa kuwa
ni ukatili wa kijinsia kwa motto huyo.
Amesema,
sheria ya mtoto ilipitishwa na serikali mwaka wa 2009, sheria hiyo
huwalinda watoto dhidi ya mazingira hatarishi na unyanyasaji na kwamba
Kama kila mtu mzima akilea mtoto mmoja, watoto (wote) wa Tanzania
watakuwa katika mazingira salama.
Amefafanua
kuwa , maelezo ya awali ya wazazi wa kijana huyo, yameweka bayana
kwamba walezi hao baada ya kumuhangaikia kwa muda mrefu ya bila kupata
nafuu, sasa wameamua kumtelekeza kijana huyo na kuamua kumfungia ndani
na kumuachia mungu kama walivyoeleza.
Akizungumzia
hilo, Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary Jama, amesema taarifa
za Ferdrick kuishi ndani ya nyumba hiyo walikuwa nazo lakini hawakuwahi
kupata taarifa za kwamba kijana huyo hatolewi nje.
Kugundulika
kwa kijana huyo kunatokana na taarifa zilizotolewa na mmoja wa
wanafamilia ambaye hakupendezwa namna kijana huyo anavyo hudumiwa na
wazazi wa mtoto huyo.
Post a Comment