Timu ya soka ya
Wales iliweka rekodi nzuri usiku wa Jumamosi katika historia ya soka
nchini humo walipotoka nyuma na kuishinda Ubelgiji katika michuano ya
Euro 2016 na hivyobasi kujikatia tiketi ya nusu fainali kwa mara ya
kwanza katika mchuano mkubwa.
Radja Nainggolan aliiweka kifua
mbele Ubelgiji mjini Lille kupitia mkwaju mkali alioupiga umbali wa
miguu 25 lakini nahodha wa Wales Ashley Williams alifunga bao la kichwa
kupitia kona na kusawazisha katika kipindi cha kwanza cha mechi.Lakini mashabiki wa Wales walifurahishwa zaidi na bao lililofungwa na Hal Robson Kanu ,ambaye ni mshambuliaji bila klabu,na kufanya mambo kuwa 2-1.
Na baada ya presha kali kutoka kwa washambuliaji wa Ubelgiji ,Wales walikifunga kidomodomo cha wapinzani wao kupitia kichwa kilichofungwa na mchezaji wa ziada Sam Vokes na hivyobasi kutinga nusu fainali dhidi ya Ureno huku wachezaji nyota wa Real Madrid Gareth Bale na Christiano Ronaldo wakijipata katika pande pinzani.
Post a Comment