Serikali ya Iraq
imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa
yaliyotokwea kutokana na shambulio la bomu ambalo limeua watu wapatao
mia 120 katika mji mkuu wa Baghadad.Katika shambujlio hilo watu mia na
hamsini walijeruhiwa vibaya wakati lori lililokuwa na milipuko
lilipolipuka nyakati za usiku karibu na msikiti katika wilaya ya
Karanda.
Mlipuko huo uliotokea katika eneo lenye shughuli nyingi
ambapo baadhi ya watu walikkuwa wakijipatia mahitaji kwa ajili ya mfungo
wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Tayari wapiginaji wa Islamic State
wamekiri kuhusika na mlipuko huo.Muda mfupi baada ya mlipuko huo Mkuu wa
majeshi ya nchi hiyo Major Generali Kadimu Shabaani alifika katika eneo
la tukio.
"
Post a Comment