Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania
Bodi ya Utalii
Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya
shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa
iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.
Shirika hilo lilikuwa likiripoti kuhusu kifo cha Guguleth Zulu, raia wa Afrika Kusini, aliyefariki akikwea Mlima Kilimanjaro.
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na
Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si
Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
ilisema.
Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.