Hifadhi ya wanyama
pori ya taifa ya Selous Kusini mwa Tanzania inatajwa kuwa huenda
ikapoteza tembo waliosalia ndani ya miaka sita ijayo iwapo hali ya
ujangili itaendelea kwa kiwango kilichopo sasa.
Ripoti ya mfuko wa
hifadhi ya wanyamapori na mazingira duniani,wwf imesema hifadhi Selous
imepoteza asilimia tisini ya tembo wake,ambapo miaka 40 iliyopita
kulikuwa na maelfu ya tembo.
Mahitaji makubwa ya nyara hizo na
nchi ya China,kwa mjibu wa ripoti hiyo inatajwa kuwa ni hali
inayochochea ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo.
Rais wa
awamu ya tano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika utawala wake
ametanga kukomesha rushwa ambayo ndiyo imekuwa ikichangia kukua kwa
vitendo vya ujangili.
"hifadhi hiyo ya Selous ni moja kati ya urithi wa dunia kufuatia kuwa na eneo kubwa la wanyama pori lililosalia Barani Afrika.bbc
Post a Comment