Serikali imesema kuwa itasambaza
madaktari bingwa katika mikoa tisa yenye uhaba mkubwa wa madaktari hao
ili kuboresha sekta ya Afya katika maeneo hayo na kuepusha gharama za
wagonjwa kusafirishwa mbali kwenda kupata huduma.Akiongea
jana bungeni Mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu,
amesema kuwa watatoa kipaumbele kwa madaktari na wahudumu wa afya ambao
wapo tayari kufanya kazi mikoani.
Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika
Mikoa ambayo itapewea kipaumbele ni ile inayoonekana ina upungufu mkubwa
wa watumishi hao ikiwemo Mkoa wa Tabora, Kigoma, Mara, Katavi, Rukwa
Simiyu na mingineyo ya Pembezoni.
Waziri Ummy ametumia nafasi hiyo
kuwaambia madaktari na wahudumu wa Afya wanaotafuta ajira serikali kuwa
hawatua na nafasi kwa Daktari ambae atataka kukaa Dar e s Salaam kwa
hiyo watatoa vipaumbele kwa wale ambao wako tayari kwenda pembezoni.
Post a Comment