Wakili wa China aliyevuliwa nguo
Mawakili wengi wa
China wamenyanyaswa,kukamatwa na hata kufungwa jela lakini picha ya
mmoja wao aliyekuwa na nguo zake zilizovuliwa na maafisa wa polisi
imevutia hisia nyingi nchini China.
Wu Liangshu alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Qingxiu akiwa amevalia koti lake na suruali ya ndani ikionekana.
Yeye
na mawakili wengine waliambia maafisa wa mahakama kwamba alishambuliwa
na maafisa watatu katika mahakama moja mbele ya majai mawili ambao
walikataa ombi lake la kutaka kuanzisha kesi katika mahakama ya wilaya
ya Nanning Mkoani Guangxi.
Bw Wu alipewa nguo nyengine lakini alijua uwezo wa kile alichokuwa akipanga kukifanya.''Asante alisema''.
Wakili
huyo baadaye alitembea kupitia mlango wa mbele akiwa amebeba nakala
zake za mahakamani akiwa na kalamu iliowekwa katika mfuko wa shati
liliposuliwa.
Baadaye alipigwa picha nje ya jengo hilo la mahakama.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.