0

Mjadala   wa    bunge  kuhusu bajeti  umezidi  kupamba moto  baaada  ya  wabunge  wa Chama Cha Mapindunzi  CCM  kutumia  muda huo   kuwasema  wale  wa  upinzani na kulaani kitendo cha  wao kutoka nje ukumbi hatua ambayo inasababisha  washindwe kuonyesha  ushiriki  wao  katika  bajeti  hiyo ambayo ni dira muhimu  kwa taifa kwa mwaka 2016/2017.

Wakitumia dakika  tano  tano  kwa kila mmoja   wabunge hao akiwemo Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera wamesema  kitendo cha wenzao   wa upinzani  kususia  mjadala huo hakileti  afya kwa wananchi  wa majimbo wanayoyawakilisha na hivyo watizame upya maamuzi yao

Ushauari  huo  unakataliwa  na  Mh  Joseph Mbilinyi  mbunge wa Mbeya mjini ambaye anasema wao wanaamini  kuwa   kuwawakilisha  wananchi  siyo lazima kuingia bungeni  na ndio maana hata  sasa wanafanya vikao  vyao vya  kuijadili bajeti hiyo  katika  ukumbi wa zamani  wa  msekwa  na watatumia mbinu zao  wanazozijuwa kuwafikishia  wananchi  wao  taarifa  za  bajeti hiyo.


Hata hivyo  kutokana  na mvutano huo  naibu  spika  Dk Tulia  Ackson  analitolea ufafanuzi   suala hilo ambapo  anasema  wabunge wa upinzani  kutoka nje wanafanya hivyo kwa utashi  wao.

Katika hatua nyingine wakichangia hotuba hiyo  Mh Ahmed Shabiby  mbunge  wa  Gairo  amesema  kwa sasa  hali  ya  fedha  mtaani  ni ngumu sana  hivyo mpango wa serikali wa kuelekeza fedha zote hazina  utazidi kuongeza machungu  huku  Mh  Oran Njeza mbunge wa Mbeya vijijini  akitaka   ofisi ya CAG  kuja na mkakati  mpya wa kudhibiti  fedha  za  umma.

Post a Comment

 
Top