Maelfu ya watu
wamejumuika pamoja katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan, katika
mojawepo ya maandamano makubwa katika kipindi cha miongo miwili, kupinga
uwepo wa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo
.
Waandamanaji
wana hasira kuhusiana na madai ya ubakaji na mauwaji ya kijana mmoja
mwanamke wa eneo hilo, yaliyotekelezwa na mwanajeshi wa zamani wa majini
wa Marekani, wanaoishi katika kisiwa hicho.
Kisa hicho kimefufua upinzani mkubwa kisiwani Okinawa dhidi ya kambi ya wanajeshi wa Marekani kisiwani humo.
Mipango ya kuondoa kambi hiyo haijafua dafu.
Post a Comment