Watu saba wamefariki na wengine 21 wamelazwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa ajabu katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma huku dalili zake zikiwa ni kutapika,kuharisha,kupata rangi ya manjano machoni na sehemu zingine na tumbo kuvimba na kujaa maji ambapo inaaminika watu wa kwanza kubainika kuugua walikula nyama vya ng’ombe aliyevunjika mguu katika kijiji cha Mwaikisabe wilayani Chemba.
Akizungumzia
kuibuka kwa ugonjwa huo ambao umezua taharuki kwa wakazi wa mkoa wa
Dodoma na maeneo ya jirani Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia
wazee na watoto mhe Ummy Mwalimu amesema tayari sampuli za ugonjwa huo
zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi huku
akiwatoa hofu wakazi wa mkoa huo ambao wanahisi huenda ukawa ni ugonjwa
wa kimeta.
Mbali
na kushambulia binadamu lakini pia ugonjwa huo umezuru wanyama wafugwao
wakiwemo mbwa na paka kwa upande wake Dk James Chalz Mganga Mkuu wa
mkoa wa Dodoma anasema bado wataalam wa magonjwa mkoani Dodoma
wanaendelea na uchunguzi huku akidai kuwa wagonjwa wanaendelea na
matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na hospitali
ya wilaya ya Kondoa.
Post a Comment