Utafiti mpya
umebaini kuwa wanawake ambao wamewahi kuugua saratani ya matiti huenda
wakanufaika na chembechembe zinazozuia ugonjwa huo kwa muda mrefu zaidi
kuliko muda wa sasa wa miaka mitano.
Utafiti huo uliofanywa na
wanasayansi kutoka Marekani na Canada umebaini kuwa kutumia dawa hizo
kwa miaka kumi badala ya mitano unapunguza uwezekano wa saratani hiyo
kurejea kwa theluthi moja.Visa vingi vya saratani ya matati husababishwa na homoni za kike zinazofahamika kama 'Oestrogen' na dawa za kuzia homoni hizo hutumia sana.
Watafiti hao wanasema matokeo ya utafiti huo huenda yakabadili matibabu kwa mamilioni ya wanawake.
Watafiti hao pia wameonya kuwa dawa za kuzuia homoni hiyo zinaathari kubwa kama kuvunjika kwa mifupa na kukosa hamu ya kujamiana.
Post a Comment