Polisi
katika kisiwa cha Pemba visiwani Zanzabar nchini Tanzania imepinga
vikali kuwa inavunja haki za binadamu kwa kuwatesa na kuwashikilia
wapinzani.
Hata hivyo limekiri kuwashikilia baadhi ya wapinzani kwa madai kwamba ni wahalifu.
Hapo
jana Muungano wa Upinzani nchini Tanzania ulitoa kauli ya kulaani
Polisi huko Pemba kwamba imekuwa ikiwapiga, kuwatesa na kuwafungulia
kesi za bandia wafuasi wa upinzani .
Muungano huo tayari umetishia
kumpeleka Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye mahakama ya kimataifa
ya ICC iwapo hataingilia kati mgogoro huo unaoendelea visiwani humo.
Kutoka
Dar es Salaam mwandishi wetu Regina Mziwanda amezungumza na Naibu
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi Zanzibar Salum Msangi na kwanza
alimuuliza hali ya usalama ikoje huko Pemba.bbc
Post a Comment