Bado michano ya mataifa ya Ulaya maarufu kama UEFA Euro 2016, imeendelea tena leo June 12 Ufaransa kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja mbalimbali, mchezo wa mwisho kuchezwa kati ya Ujerumani dhidi ya Ukraine ndio mchezo uliokuwa unatarajiwa kutazamwa na mashabiki wengi.
Ujerumani ambao walicheza mchezo wao kwanza wa Euro 2016 walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na Shkodran Mustafi dakika ya 19 na Bastian Schweinsteiger dakika ya 90, huu ni mchezo ambao ulionekana kama wa uapnde mmoja.
Kwa muda wote wa dakika 90 Ukraine walionekana kuwa wanyonge na Ujerumani kuzidi kumiliki mpira kwa asilimia 63, huku Ukraine wakionekana wanyonge kwa kumiliki mpira kwa asilimia 37, kwa sasa Ujerumani wanaongoza Kundi C kwa kuwa na point 3 na magoli mawili wakifuatiwa na Poland wenye point tatu na goli moja.
Post a Comment