0

Ndugu wa wakaazi wa Arusha na haswa vijana napenda kuchukua nafasi kuwatakia mfungo mwema wa MWEZI mtukufu wa Ramadhani

kama ilivyoandika katika kitabu kitakatifu kwa waislam zipo nguzo tano nguzo mojawapo nikufanya ibada ya kufunga mwezi wa Ramadhani

nivizu Kwa tusio waislam kuitumia nafasi hii vizur kufanya mambo ambayo hayatawakwaza  wenzetu kwenye kufanikisha Ibada yao

kwa wafanyabiasha wa jiji la Arusha tusitumie nafasi hii kupandisha bidhaa bei ilikupata faida kubwa hii itakuwa ni dhambi kubwa sana kuwakomoa watu wanaofanya ibada nivizur tukafanya  biashara kwa haki kama tulivyokuwa tunafanya mwanzo

Kwa hapa Arusha najua viongozi wetu wa serikal watasaidia kuweka mambo sawa haswa kwenye masoko yetu makubwa kama soko kuu na kilombero

Uvccm inawatakia vijana wote nawakazi wa Arusha Ramadhani njema wakati wa ibada yetu ya funga tuiombee nchi yetu na haswa raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli aendele kutekeleza vyema majukumu yake .

Asante sana kunisikiliza Ramadhani karimu

     imetolewa na

Mwenyekiti Uvccm wilaya ya Arusha mjini
Martin.D.Munisi

Post a Comment

 
Top