kutoka gazeti la Mwananchi, yenye kichwa cha habari ‘simu bandia zapata soko Msumbiji, Congo’. ‘simu bandia zapata soko Msumbiji, Congo’.
Gazeti
hilo limeripoti kuwa Siku mbili baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA) kuzima simu feki, wafanyabiashara wa simu hizo wamepata soko
jipya katika nchi za Msumbiji na Congo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na gazeti hilo, baadhi ya vijana waliokutwa
wakizunguka madukani kuzikusanya, walisema wanazinunua na kuzisafirisha
kwenda huko kwa ajili ya kuziuza kwa watumiaji. Walisema katika nchi
hizo kuna soko kwa sababu zinakamata mawasiliano kama kawaida.
Gazeti hilo limemnukuu Lawrence Kyondo
ambapo amesema wanazinunua kwa bei ya makubaliano na kwenda kuziuza
katika soko la nje……….>>>’hatujaanza hii biashara leo, siku
nyingi isipokuwa wenye maduka walikuwa bado wagumu kuziuza wakidhani
hazitazimwa’
Post a Comment