Urusi inasema kuwa
Rais Erdogan wa Uturuki ameomba msamaha kwa hatua ya taifa lake,
kuidungua ndege ya kivita ya Urusi karibu na mpaka na Syria mwaka jana.
Katika
ujumbe ulioandikwa ndani ya barua hadi Kremlin kwa Rais Putin, Bwana
Erdogan alielezea masikitiko yake makubwa kwa kile kilichofanyika, huku
akisema anataka kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo
mawili.Uturuki bado haijatoa maelezo kuhusiana na barua hiyo.
Udunguaji wa ndege hiyo uliibua mgongano mkubwa wa kisiasa, uliopeleekea Urusi kuiwekea Uturuki vikwazo vya kibiashara ambavyo vingeondolewa tu baada ya Rais Erdogan kuomba msamaha.
Post a Comment