TANZANIA itaanza kuuza masafa ya mawasiliano kwa njia ya mnada kuanzia mwakani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema hayo jana baada ya kumaliza
mkutano wake na Mtendaji Mkuu wa Nchi wanachama wa Mawasiliano katika
Jumuiya ya Madola, Dk Shola Taylor.“Kuanzia
mwakani mnada wa masafa utaanza, zoezi hilo ni jipya hatuwezi kufanya
makosa, nina imani tutapata fedha za kutosha, ” alisema.
Waziri Mbarawa alisema masafa hayo
yalipatikana baada ya Tanzania kutoka analojia kwenda digitali ambapo
masafa 700- 816 yako wazi.
Alisema baadhi ya nchi barani Afrika
zimeanza kuuza masafa kwa njia ya mnada na sasa Tanzania itaanza mwakani
na kuongeza kuwa nchi za Ghana na Nigeria zimefanikiwa katika hilo na
Tanzania inataka kufanya kitu kutokana na mafanikio hayo.
Alisema watakaonunua masafa watatakiwa
kuyatumia, vinginevyo wanaweza kunyang’anywa masafa hayo na kuwa
wanataka kujipanga vizuri ili sekta hiyo ipate fedha na anaamini
Tanzania itafanikiwa katika hilo.
Post a Comment