0

Magu. Mteni wa kabila la Wasukuma wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, John Nyanza (70), amefariki dunia.

Katibu wa Umoja wa Watemi wa Usukuma, Charles Itale, amesema jana kuwa mtemi huyo alifariki dunia Juni 15, mwaka huu  majira ya alfajiri kwa ugonjwa wa saratani.

 “Mtemi mwenzetu alifariki dunia katikati ya wiki iliyopita wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC),” amesema Itale.

Utemi wa Usukuma ambao makao makuu yake yapo Bujora, unaundwa na mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza.

Post a Comment

 
Top