Burudani leo ilikuwa hivyo ndani ya uwanja wa wilaya ya Liwale
Mchezaji wa timu ya Mpengele fc akiitwa na mwamuzi wa mchezo baada ya kufanya makosa ya kupiga mpira baada ya mwamuzi kupiga filinbi
JUNE 29 ligi ya Liwale super cup leo kulikuwa na mchezo
kati ya LIKOMBORA FC Vs MPENGELE FC Mchezo uliochezwa uwanja wa wilaya
ya Liwale.
katika mchezo wa leo timu zote zilionesha uwezo
lakini Timu ya Mpengegele fc iliendeleza kutoa dozi na leo waliweza
kuichapa timu ya Likombora fc mabao 2 bila magoli yaliofungwa kipindi cha
pili na HABIBU MUTWE dakika ya 67 na MIKIDADI MOLA dakika ya 75.
Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo LIKOMBORA FC 0-2 MPENGELE FC
Katika ligi hii Mpengele fc ndio timu pekee iliyofikisha point 6 kwa michezo miwili huku Likombora fc wamefungwa mechi 2.
Namo dakika ya 80 ya mchezo kocha wa timu ya Likombora fc alipewa kadi nyekundi baada ya kutoa lugha chafu kwa mwamuzi wa mchezo huu hii ni mara ya kwanza kocho kuonesha kadi nyekundi kwenye ligi hii.
Kapteni wa Likombora fc Abdala Kiindikwa alisema mchezo wa leo walicheza kwa kupaniki sana wakiwa na lengo la kutaka ushindi katika mchezo wa leo nae Mikidadi Mola kapteni wa Mpengele fc alisema mchezo ulikuwa mzuri kwa pande zote na amefuhisha na ushindi walioupata leo na kuweza kukusanya pointi 3 muhimu na kuifanya Mpengele fc kuweza kutimiza pointi 6 kwa kuweza kushinda mechi mbili walizocheza.
Kesho kutakuwa na mchezo wa aina yake kati ya timu ya Mihumo fc Vs Hawili fc mchezo utakaotimua vumbio uwanja wa wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.
Post a Comment